Friday, January 2, 2015

SPORTS AND GAMES


Wachezaji waliounda timu ya Chuo cha Ardhi Tabora iliyocheza na
timu kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC), katika mechi iliyochezwa
katika uwanja wa Chuo cha Ardhi Tabora.

Katika chuo cha Ardhi Tabora kuna aina mbalimbali za michezo inayofanyika, lakini
michezo ambayo imekuwa ikiongoza kwa kuwa na washiriki wengi zaidi ni Mpira wa miguu(football), ukifuatiwa na Mpira wa pete(Basketball).
       Katika mwaka wa masomo 2012/2013, Mheshimiwa Mkuu wa chuo, Ndg. Biseko Musiba aliuwezesha mchezo wa mpira wa miguu kwa kununua mipira, nyavu na kuanzisha mashindano yaliyojulikana rasmi kama "Arita Intercourses Sports League". Katika ligi hiyo zawadi mbalimbali zilitolewa kwa wachezaji bora, timu bora, timu yenye nidhamu, wachezaji waliotetea timu kwa kiwango cha juu, pamoja na kutolewa Kombe kwa timu-mshindi.
        Pamoja na ligi hiyo, tunamshukuru Mkuu wa chuo kwa kutuunga mkono kwa kufadhili ziara za kimichezo katika vyuo mbalimbali, hasa TTC (Chuo cha Ualimu Tabora) na TPSC (Tanzania Public Services College, maarufu kama UTUMISHU WA UMMA). Ufadhili huo ulifanyika kwa timu ya mpira wa miguu kwa Wavulana na Timu ya mpira wa mikono kwa Wasichana.
        Michezo, kama ilivyotajwa na wataalamu kuwa inaboresha afya za washiriki na kuimarisha uwezo wa kiakili, ni moja ya nyanja zinazostahili kupewa kipaumbele hasa ikizingatiwa kuwa chuo kina maeneo ya kutosha kwa ajili ya michezo hiyo.
        Katika matumaini yetu, hata michezo mingine itaweza kupewa vipaumbele, hasa ile inayoonokana kupata washiriki wengi. Shukrani ziwaendee wote wanaojitoa ipaswavyo katika kufanikisha michezo katoka chuo cha Ardhi Tabora, lakini shukrani za pekee ziende kwa Mh. Mkuu wa chuo, Ndg. Biseko Musiba kwa jitihada zake. Tunamwombea maisha marefu ili pia aendelee kukijenga chuo kwa ufanisi wa hali ya juu.

No comments:

Post a Comment